Wakina mama wajasiriamali wakiwa katika mafunzo hayo |
Wanawake Wajasiriamali wakisubiri kuingia katika mafunzo hayo |
Na Dotto
Mwaibale
NAIBU Waziri wa
Kazi na Ajira Dk.Makongoro Mahanga amesema ukosefu wa ajira hapa nchini ni
jambo tete ambapo kila mtu anatakiwa kujiajiri mwenyewe ili kukabiliana na sua
hilo.
Hayo
aliyasema wakati akifungua mafunzo ya ufundi stadi na ujasiriamali kwa wanawake
wa Kata ya Kipawa Dar es Salaam leo.
Alisema
suala la upatikanaji wa ajiri haipaswi kuachiwa kwa serikali pekee bali kila
mtu mmoja mmoja alipo anatakiwa kupambana na suala hilo kwa kujiajiri kama wanavvyo
fanya wanawake hao wa Kata ya Kipawa.
“Kazi ya
Serikali ni kuhakikisha inawapunguzia mzigo wananchi kwa kujenga Zahanati,
Madarasa, barabara na si kuwanunulia chakula wananchi ambao ni wajibu wao”
alisema Dk.Mahanga.
Alisema
suala la ajira linachangamoto kubwa si kwa Tanzania bali dunia nzima isipo kuwa
linatofautiana kimazingira kwani kwa nchi zilizoendelea wanapo sema hawana
ajira ni katika sekta za viwanda,
serikali na katika sekta rasmi tofauti na hapa kwetu.
Alisema kwa
hapa nchini suala hili ni tete kwa sababu hatuna viwanda vya kutosha na ajira
zinazotolewa serikali ni chache hivyo njia pekee ya kujikwamua ni kujiajiri
wenyewe kwa kujiingiza katika ujasiriamali.
No comments:
Post a Comment