HALI si shwari katika Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Bavicha), baada ya kuelezwa kuwa limemvua uongozi na
kumfukuza uanachama Makamu Mwenyekiti wake, Juliana Shonza.
Habari zilizopatikana jana jioni zilieleza kuwa
mbali na Shonza, baraza hilo pia limewafukuza uanachama aliyekuwa
mgombea wa ubunge Jimbo la Kibaha Mjini, Habib Mchange na aliyekuwa
akigombea ubunge Jimbo la Mbozi Mashariki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2010, Mtella Mwampamba.
Habari kutoka ndani ya baraza hilo zimeeleza kuwa
mbali ya viongozi hao, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mbeya,
Gwakisa Mwakasendo naye amepewa onyo kali.
Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha kilichofanyika Mbezi, Dar es Salaam juzi.
Uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha kilichofanyika Mbezi, Dar es Salaam juzi.
Habari hizo zimeeleza kwamba viongozi hao
wamefukuzwa kwa tuhuma mbalimbali. Hata hivyo, Shonza hakuwapo katika
kikao hicho.
Akizungumzia madai hayo, Shonza alisema jana
kwamba hata yeye amesikia taarifa hizo katika mitandao ya kijamii,
lakini hana taarifa kwa kuwa hajapata barua yoyote.
“Mimi sikuwepo kwenye kikao lakini nimezisikia
taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii na hata barua yenyewe ya
kufukuzwa sijaipata, hivyo siwezi kusema chochote juu ya hilo,” alisema
Shonza.
Kwa upande wake, Mchange alisema kwamba alihojiwa juzi katika kikao hicho na kuelezwa kuwa anakivuruga chama.
Kwa upande wake, Mchange alisema kwamba alihojiwa juzi katika kikao hicho na kuelezwa kuwa anakivuruga chama.
Alisema baada ya kuelezwa hivyo aliomba mwongozo
wa Chadema, lakini hakupewa na baada ya kuhojiwa aliamuriwa kutoka nje
ya kikao hicho.
“Baada ya kutolewa niliondoka lakini niliomba
nisomewe katiba, lakini sikukubaliwa na hivyo tumesikia tu baada ya
kuondoka kwamba uamuzi wa kutufukuza ulifikiwa,” alisema Mchange.
Alisema aliitwa kwenye kikao hicho akiwa mjumbe wa Bavicha, lakini alipofika ndipo akakutana na suala hilo la kuhojiwa kuhusu mambo ya chama.
Alisema aliitwa kwenye kikao hicho akiwa mjumbe wa Bavicha, lakini alipofika ndipo akakutana na suala hilo la kuhojiwa kuhusu mambo ya chama.
“Hizo taarifa za kufukuzwa nimezisikia, lakini
nikwambie tu Heche (John, Mwenyekiti wa Bavicha), hawezi kunifukuza
uanachama kwa kuwa mimi si mwanachama wa Bavicha, bali ni mwanachama wa
Chadema,” alisema Mchange.
Akizungumzia suala hilo, Mwampamba alisema kwamba
aliitwa kwenye kikao hicho baada ya kutumiwa ujumbe wa kualikwa, lakini
alipofika alitakiwa kusubiri nje ya ukumbi na baadaye aliitwa ndani.
“Ilipofika saa nne usiku niliitwa na kuelezwa kuwa
kuna tuhuma ambazo natakiwa kujibu. Nilikataa na kuwaeleza kuwa sina
imani na mwenyekiti pamoja na katibu, hivyo mabaunsa wakanitoa nje,”
alisema Mwampamba.
Alisema amesikia taarifa za kufukuzwa kwenye
mitandao ya kijamii, lakini hajashtushwa kwa kuwa kuna utaratibu ambazo
lazima zifuatwe kabla ya hatua hiyo.
Alipotakiwa kuthibitisha habari hizo jana, Heche alisema amejipanga kutoa ufafanuzi leo katika mkutano wake na waandishi wa habari.Mwananchi.
Alipotakiwa kuthibitisha habari hizo jana, Heche alisema amejipanga kutoa ufafanuzi leo katika mkutano wake na waandishi wa habari.Mwananchi.
No comments:
Post a Comment