WAZIRI mkuu mstaafu John Samwel Malecela, ametaka
kuchukuliwa kwa hatuia za kuwafikisha mahakamani watu wotewenye fedha ambao
hazijulikani namna walivyopata.
Akizungumza katika kipindi cha dakika 45 leo kinachorushwa
kila siku ya jumatatu na kituo cha Luninga cha ITV malelecela amesema watu hao
wanapaswa kuhojiwa kwa ajili ya kujua vyanzo vyao kama havihusiani na ufisadi
unaoendelea nchini.
Amesema alipokuwa nje ya nchi alishangaa kuambiwa na wenyeji
wake kuwa kuna mtanzania aliyefika huko na kununua gari aina ya Range
Rover kisha akapakia katika ndege kitu
alichoeleza si cha kawaida hata katika nchi zilizoendelea
Akizungumzia elimu Malecela amesema hatua ya kuwepo kwa
shule za sekondari katika kila kata linafaa kupongezwa na kinachopaswa ni
kuiboresha zaidi kwa ajili ya kuwasaidia vijana
Alitolea mifano ya baadhi ya shule za kata zilizoweza
kuingia katika shule 20 bora za kitaifa na kueleza hilo si jambo la kupuuzwa.
Kuhusu umeme alisema serikali ya awamu ya kwanza iliamini
katika umeme wa vyanzo vya maji na sasa viongozi waliopo wana wajibu wa
kutafuta umeme mbadala itakayowezesha nchi kufanya kazi kwa muda wote
Amesema kama watanzania wataamua kujitoa kwa kununua umeme
jua leo hii kusingekuwa na kelele za kupigania umeme wa tanesco
No comments:
Post a Comment