Tuesday, November 13, 2012

MKUTANO WA KUJADILI NAMNA YA KUTUMIA NAMBA MOJA KUPIGA MITANDAO YOTE KUFANYIKA JIJINI DAR

Mkurugenzi  Mtendaji wa Mamlaka ya  Mawasiliano Tanzania Prof John Nkoma akizungumza na waandishi wa habari leo katika  Makao makuu ya ofisi hizo ambapo alizungumzia juu ya kuwepo kwa Mkutano wa siku mbili wa kujadili juu  ya namna ya  kutumia namba moja ya simu kwenda namba nyingine.
Prof Nkoma amesema kuwa  zoezi hilo likifanikiwa itamwezesha mteja  kutumia namba moja tu na kuweza kuwasiliana na mitandao mingine.

Mkutano huo uatafanyika siku ya Tarehe 15 na 16 katika ukumbi wa mikutano mlimani Cty.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano huo wakiwa Kazini.

No comments:

Post a Comment