Vyama vikubwa vya Upinzani vya Rwanda vilivyo uhamishoni vimemshutumu
Rais wa Rwanda, Paul Kagame kuwa anampango wa kufanya mabadiliko ya
vifungu vya katiba ili awanie Urais kwa Muhula wa tatu.
Chama
cha Unified Democratic Forces (FDU) na Rwanda National Congress(RNC)
walifanya mkutano wa pamoja mjini Johannesburg nchini Afrika kusini
mkutano uliomalizika mwishono mwa Juma.
Vyama
hivyo vimesema kuwa mkutano huo umelenga kukemea mipango hiyo ya Rais
Kagame na kutoa wito kwa Raia wa Rwanda , nchi jirani na Jumuia ya
kimataifa kukemea jitihada hizo za Kagame za kuendelea kubaki
madarakani.
Kagame anatarajiwa kumaliza Muhula wake wa pili mwaka 2017.
Taarifa
za vyombo vya habari vya ndani ya nchi hiyo vinasema kuwa mwanzaoni mwa
mwezi huu, Kagame aliwaagiza Maseneta watatu nchini humo kuhakikisha
kunakuwepo na mabadiliko baada ya mwaka 2017.
hatua
hiyo imepokelewa kwa namna tofauti huku Waangalizi kadhaa wakisema
Chama tawala kitaitisha Kura ya maoni juu ya mabadiliko ya Katiba ili
kutoa nafasi kwa Kagame kuwania tena urais.
Imeandikwa na Lizzy Anneth Masinga via RFI
No comments:
Post a Comment