Na Bryceson Mathias
KWA matokeo
Bomu ya kidato cha nne ya Mwaka 2012, ni wakati muafaka sasa, Serikali
inatakiwa ijihoji na kujisikia aibu inatengeneza taifa Bomu la aina gani
kupitia sekta ya Elimu? Hii ni kwamba kama ningekuwa Shukuru Kawambwa
(pichani kulia) au Philipo Mulugo, ningejiuzulu nipishe wengine nao
wajaribu.
Kwa matokeo
mabaya na ya kusikitisha ya Kidato cha nne yaliyotangazwa kwa mwaka
2012, ni budi Serikali iepuke usanii na ikubali kukosolewa na wachambuzi
wa Elimu na ijihoji na kujitathini na kuona, huko mbele inatengeneza
na kuzalisha Taifa Bomu la aina gani nchini? .
Usanii
ninaousema ni pamoja na madudu yaliyobainika kuandikwa na wanafunzi
kwenye majibu hali inayotuoonesha kwamba, alivyo mfalme ndivyo walivyo
wafuasi wake, kwamba maana ya kuwa yalivyo matokeo ya wanafunzi wetu
nchini yanatuonesha namna ya viongozi na watalaam wa elimu tulionao.
Ninasema hivyo
kwa sababu wadadisi wa mambo wanasema, likiwepo Taifa Bomu, huzaa
Viongozi Bomu, na Viongozi Bomu hutoa mazao Bomu, ambapo Mazao hayo Bonu
nayo hutoa utendaji Bomu, na kama utendedaji utakuwa Bomu, basi hakuna
maendeleo na ustawi wa Taifa na wananchi wake.
Hivi karibuni
kupitia kwa Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia NCCR-Mageuzi alilalamikia
Udhaifu wa Sekta ya Elimu nchini, lakini kuna watu ambao watoto wao
hawasomi kwenye shule za kata labda nje au kwenye Shule St. zinazofanya
vizuri kutokana na uwezo wao waliipuuza wakisema serikali inafanya
mapitio.
Mambo ya
muhimu yakizuiwa kwa madai ya kufanya mapitio, maana yake ni kwamba
hayastahili kushughulikiwa kwa dharura hali inayokinzana na Hoja ya
Mbatia akitaka liwe jambo la Dharura na Muhimu linalopaswa kupewa
kupaumbele lifanywe Haraka.
Kinachoonesha
kama tunao watalaam wa elinu kwenye sekta hiyo basi wakati wakiwafunisha
watalaam wetu hao wakati wa kufundisha ubaoni, labda walipokuwa
wakiandika na Chaki zao ubaoni, Chaki hizo ziliznguka chini hivyo
walishindwa kuandika wakati wa kuwafundisha watoto wetu.
Kama chaki za
watalaam na viongozi hao zilianguka, ni dhahiri kuwa na hata baadhi ya
walimu wetu kwenye Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo Chaki zao
inaonesha zimeanguka kiasi cha kutupatia matokeo duni yanayowapendelea
vigogo wenye uwezo wa kuwapeleka watoto wao shule za St.
Matokeo haya
ni dhahiri yamewaumbua walioifuja hoja hii na licha ya kuwapatia aibu
kwa nyakati fulani nilimshangaa Waziri wa Elimu Shukuru kawambwa alikuwa
anacheka badala ya kusikitika au kulia kabisa.
Nakasirishwa
na baadhi ya viongozi ambao wakishauliwa juu ya elimu wanajifanya
wanajua wakati hawaju huku mambo kwa watoto wetu yakienda mrama na ya
watoto wao yakienda vizuri raha mustarehe!!.
Kama
serikali kwa macho yake imeshuhudia wanafunzi wasiojua kusoma, kuandika
na kuhesabu wakifaulu Mtihani wa Darasa la Saba, na wazazi wao kukataa
kuwaruhusu watoto wao kuendelea na kidato cha kwanza Mfano Bahi Dodoma
mzazi alikataa mwanae aisome kwa na Mbeya ambako Mbunge aliliambia
Bunge. Je kwa msingi huo tuna sababu ya kuwa na Kawabwa na Mulugo
wizarani?
Aidha
ni ushauri wangu Wizara ya Elimu na Ufundi tangu Makao Makuu ya Elimu
wizani hadi wilayani ifumuliwe na kuwekwa nyuso mpya zisizo za usanii wa
sekta hiyo, maana sasa ndiyo tunabaini malalamiko ya walimu.
0715-933308
No comments:
Post a Comment