Alisema Oktoba 19 mwaka huu
waziri wa wizara hiyo, John Magufuli alitoa agizo kuwa hadi Novemba 15
mwaka huu itakuwa siku ya mwisho ya kusajiliwa magari yote ya Umma
kulingana na sheria na taratibu za nchi.
Akifafanua, Ndunguru alisema
magari yote ya Umma katika wizara, Idara za serikali na taasisi za Umma
yanayotumia nambaza kiraia, magari hayo yanapaswa kusajiliwa kwa
utaratibu uliowekwa na Serikali ambao unataka magari yote ya Umma kuwa
na namba zifuatazo, magari ya Serikali Kuu yatakuwa na mamba za ST,
Serikali za Mitaa namba za SM, Mashirika ya Umma namba za SU na yale
yaliyotolewa na Washirika wa Maendeleo kwa ajili ya miradi
wanayoisaidia, namba za DFP.
Mengine ni yale ya vyombo maalum kama Jeshi (JW), Polisi (PT), na Magereza ambao wataanza kutumia namba mpya za MT.
Ndunguru alisema baada ya agizo
serikali itaendesha msakao mkali wa kukamata magari ambayo yatakuwa bado
hayajasajiliwa kwa namba za serikali.
“Sheria ya usalama barabarani
ya mwaka 1973 kifungu Na. 30 na iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004
inaipa wizara ya ujenzi kusajili na kutunza kumbukumbu za magari yote ya
Serikali ambayo yatapewa namba zitakazotanguliwa na JW, PT, ST (sheria
na 62), na DFP (GN. No.517 ya Novemba 29, 2002”alifafanua Ndunguru.
Ndunguru aliwatahadharisha wote
ambao wana magari ya Umma, ambayo bado yanatumia namba za kiraia
kubadili usajili huo, haraka ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kinidhamu
na kisheria kwa kufikishwa mahakani kwa makosa ya jinai.
No comments:
Post a Comment